Afisa maendeleo ya jamii msaidizi daraja la ii Jobs in Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Tanzania vacancies in Tanzania at Halmashauri ya Manispaa ya Musoma


POST AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II - 1 POST

POST CATEGORYS SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE, COMMUNITY AND SOCIAL
DEVELOPMENT
EMPLOYER Halmashauri ya Manispaa ya Musoma
APPLICATION TIMELINE 2020-12-31 2021-01-13
JOB SUMMARY NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES

i.Kuratibu shughuli zote za maendeleo ya jamii katika Kijiji zikiwemo za
wanawake na watoto na zikizingatia jinsia;

ii.Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia,
kutathmini mipango/miradi ya maendeleo;

iii.Kuhamasisha na kuwawezesha wanachi kupanga na kutekeleza kazi za maendeleo
ambazo ni pamoja na usafi wa mazingira, ujenzi wa nyumba bora vijijini, ujenzi
wa shule, zahanati, majosho, barabara za vijijini Feeder Roads, uchimbaji wa
visima vifupi na uchimbaji wa marambo;

iv.Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga mbinu za kutatua vikwazo vya
maendeleo hasa vya maji na nishati kwa kuwa na miradi ya uvunaji wa maji ya
mvua, majiko sanifu na matumizi ya mikokoteni;

v.Kutoa na kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwa viongozi wa kijiji na vikundi
mbalimbali vya maendeleo kijijini kuhusu-

-Utawala bora na Uongozi

-Ujasiriamali

-Mbinu shirikishi jamii na kazi za kujitegemea

-Chakula bora na lishe

-Utunzani na malezi bora ya watoto

vi.Kuwa kiungo kati ya wanakijiji Afisa Mtendaji wa Kata na watumishi
wengine wa Serikali katika kutekeleza shughuli za maendeleo;

vii.Kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za kujitegemea;

viii.Kuwawezesha wananchi kubaini na kuratibu rasilimali zilizopo na kuzitumia
katika miradi ya kujitegemea;

ix.Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kuwasaidia wananchi kutumia takwimu na
kumbukumbu mbalimbali za kijiji;

x.Kuwawezesha viongozi wa vijiji kutumia mbinu shirikishi jamii kuandaa ratiba
za kazi na mipango ya utekelezaji;

xi.Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya jamii kila mwezi kwa
uongozi wa kijiji na kwa Afisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata;

xii.Kuhamasisha na kuwezesha jamii kuona umuhimu wa kuthamini mazingira kwa
kutumia mazingira kwa njia endelevu na hasa kulinda na kuhifadhi vyanzo vya
maji kwa matumizi ya vizazi vya sasa na vya baadae;

xiii.Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo;

xiv.Kuratibu shughuli za Mashirika na Asasi zisizo za Kiserikali na za
kijamii;

xv.Kuratibu shughuli za kupambana na UKIMWI.

QUALIFICATION AND EXPERIENCE

Kuajiriwa wenye cheti cha mafunzo ya miaka miwili katika fani ya Maendeleo ya
Jamii kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya Buhare na Rungemba au Vyuo
vingine vinsvyotambuliwa na Serikali.

REMUNERATION TGS B

Login to Apply
Please see how to apply below



Apply Today Through









URL Link to Apply


Afisa maendeleo ya jamii msaidizi daraja la ii Jobs in Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Tanzania vacancies in Tanzania at Halmashauri ya Manispaa ya Musoma


Thank you very much for Visiting Mkaguzi Blog