Afisa maendeleo ya jamii msaidizi daraja ii Jobs in Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Tanzania vacancies in Tanzania at Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu


POST AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA II - 1 POST

POST CATEGORYS SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE, COMMUNITY AND SOCIAL
DEVELOPMENT
EMPLOYER Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu
APPLICATION TIMELINE 2021-02-19 2021-03-04
JOB SUMMARY NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES

i.Kuratibu shughuli zote za maendeleo ya jamii katika Kijiji zikiwemo za
Wanawake na Watoto na zikizingatia jinsia;

ii.Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia,
kutathmini mipango/miradi ya maendeleo;

iii.Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za
maendeleo ambazo ni pamoja na usafi wa mazingira, ujenzi wa nyumba bora
vijijini, ujenzi wa Shule, Zahanati, Majosho, barabara za vijijini Feeder
Roads, uchimbaji wa visima vifupi na uchimbaji wa marambo;

iv.Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga mbinu za kutatua vikwazo vya
maendeleo hasa vya maji na nishati kwa kuwa na miradi ya uvunaji wa maji ya
mvua, majiko sanifu na matumizi ya mikokoteni;

v.Kutoa na kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwa viongozi wa Kijiji na vikundi
mbalimbali vya maendeleo kijijini kuhusu-

-Utawala Bora na Uongozi

-Ujasiriamali

-Mbinu shirikishi jamii na kazi za kujitegemea

-Chakula bora na lishe

-Utunzani na malezi bora ya watoto

vi.Kuwa kiungo kati ya wanakijiji Afisa Mtendaji wa Kata na watumishi
wengine wa Serikali katika kutekeleza shughuli za maendeleo;

vii.Kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za kujitegemea;

viii.Kuwawezesha wananchi kubaini na kuratibu rasilimali zilizopo na kuzitumia
katika miradi ya kujitegemea;

ix.Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kuwasaidia wananchi kutumia takwimu na
kumbukumbu mbalimbali za kijiji;

x.Kuwawezesha viongozi wa vijiji kutumia mbinu shirikishi jamii kuandaa ratiba
za kazi na mipango ya utekelezaji;

xi.Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya jamii kila mwezi kwa
uongozi wa kijiji na kwa Afisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata;

xii.Kuhamasisha na kuwezesha jamii kuona umuhimu wa kuthamini mazingira kwa
kutumia mazingira kwa njia endelevu na hasa kulinda na kuhifadhi vyanzo vya
maji kwa matumizi ya vizazi vya sasa na vya baadae;

xiii.Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo;

xiv.Kuratibu shughuli za Mashirika na Asasi zisizo za Kiserikali na za
kijamii;

xv.Kuratibu shughuli za kupambana na UKIMWI.

QUALIFICATION AND EXPERIENCE

Wahitimu wa Kidato cha Nne au cha Sita wenye Stashahada ya Maendeleo ya Jamii
kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Buhare au Rungemba au Vyuo vingine
vinavyotambuliwa na Serikali.

REMUNERATION TGS C

Login to Apply
Please see how to apply below



Read and Apply Now Through









URL Link to Apply


Afisa maendeleo ya jamii msaidizi daraja ii Jobs in Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Tanzania vacancies in Tanzania at Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu


Thank you and dont forget to visit again Mkaguzi Blog