JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.
Na EA.7/96/01/I/39 10
Mei, 2016
TANGAZO LA
NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika
Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi
wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka
2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi
zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika
Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira
Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo
wa kujaza nafasi 188 kwa ajili ya
Wizara, Taasisi zinazojitegemea na mamlaka za Serikali za Mitaa kama
inavyoonyesha hapa chini.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA
KAZI ZOTE.
i.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri
usiozidi miaka 45
ii.
Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa. iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma
na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe
barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe
ipasavyo.
iv. Waombaji
waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na
majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v.
Maombi
yote yaambatane na vyeti vya
taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa
wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika.
-
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates. - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na
VI
-
Computer Certificate
- Vyeti
vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-
Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi.
Testmonials”,
“Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne
na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania
wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na
NECTA). viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix.
Waombaji kazi
ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa
umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC.
45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x.
Uwasilishaji wa
taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi.
Mwisho wamaombi
ni tarehe 24 Mei, 2016. xii. Aidha,
uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi
yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa
Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani
hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment
Portal’)
xiv. MUHIMU: KUMBUKA KUWEKA (ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI. ANUANI YA BARUA HIYO
IELEKEZWE KWA KATIBU, OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA S.L.P 63100 DAR ES SALAAM.
1.0 AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II
(BEEKEEPING OFFICER II) – NAFASI-
5(LINARUDIWA)
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
•
Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.
•
Kutangaza Sera na Sheria za ufugaji nyuki.
•
Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.
•
Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki. Kupanga na kupima ubora wa
mazao ya nyuki.
1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada katika
fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya
Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.
1.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya
Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
2.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 31
2.1 MAJUKUMU YA KAZI (LINARUDIWA)
• Kuendesha
magari ya abiria, magari madogo na malori
• Kuhakikisha
gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi
wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,
• Kufanya
matengenezo madogo madogo katika gari,
• Kutunza
na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye Cheti cha
Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na
uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha
ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja la II (Trade test II).
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS. Akwa mwezi.
3.0
MPISHI DARAJA LA II (COOK II ) NAFASI – 7(LINARUDIWA)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia
Wazee na Watoto. Wapishi hawa watafanya
kazi ya kuwapikia wanachuo katika vyuo vya maendeleo ya wananchi
3.1
MAJUKUMU YA KAZI
• Kuandaa
chakula cha wanachuo kulingana na Menyu na idadi ya wanachuo
• Kupika
chakula cha wanachuo
• Kutoa
ushauri kwa uongozi wa chuo kuhusu chakula cha wanachuo.
• Kusimamia
jiko.
3.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu mafunzo ya cheti
yasiyopungua mwaka mmoja katika moja ya fani ya “food Production” yatolewayo na
vyuo vya Forodhani (Dar es Salaam),Masoka (Moshi), Arusha Hotel, Y.M.C.A
(Moshi), VETA (mikumi) na Vision Hotel (Dar es Salaam) kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na serikali.
3.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGSCkwa mwezi.
4.0 MLINZI - NAFASI- 15(LINARUDIWA)
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kuhakikisha
kwamba mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya
idhini.
• Kuhahikisha
kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.
• Kulinda
usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.
• Kuhakikisha
kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi.
• Kuhakikisha
kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya
hivyo.
• Kupambana
na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile, moto, mafuriko
n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile, moto, mafuriko n.k
na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika.
• Kutoa
ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.
4.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato
cha Nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka
katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
4.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A
5.0 AFISA MISITU DARAJA LA II (FORESTRY OFFICER
GRADE II) –NAFASI- 4(LINARUDIWA)
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kusimamia
upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu.
• Kusimamia
uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi
hekta 10,000.
• Kufanya
utafiti wa misitu.
• Kutekeleza
Sera na Sheria za misitu.
• Kuendesha
mafunzo ya Wasaidizi Misitu.
• Kukusanya
takwimu za misitu.
• Kufanya
ukaguzi wa misitu.
• Kupanga
na kupima madaraja ya mbao.
• Kudhibiti
leseni na uvunaji wa miti.
• Kutoa
ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya miti
kwa wananchi.
• Kufanya
ukadiriaji wa rasilimali za misitu.
• Kupima
maeneo na kuchora ramani za misitu.
5.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya
Misitu kutoka chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine
vinavyotambuliwa na Serikali.
5.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya
Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa
mwezi.
6.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI-
5(LINARUDIWA)
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya
doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi na mbuga za wanyamapori.
• Kusimamia
utekelezaji wa taratibu za uwindaji na utalii.
• Kutekeleza
kazi za maendeleo katika Mapori ya Akiba.
• Kuhakiki
ulinzi wa nyara za Serikali.
• Kuhakiki
vifaa vya doria.
• Kudhibiti
usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya nchi.
• Kudhibiti
matumizi ya magari ya doria.
• Kuratibu
uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba.
• Kusimamia
uwindaji wa kitalii.
• Kudhibiti
na kusimamia umilikaji wa nyara.
• Kuweka
mikakati ya kudhibiti moto mkali.
• Kukusanya
takwimu za wanyamapori na mimea.
6.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato
cha IV au Kidato cha VI, wenye stashahada ya Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka au
chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
6.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B na C kwa mwezi.
7.0 MFUGAJI NYUKI MSAIDIZI DARAJI LA II –
NAFASI – 5(LINARUDIWA)
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kusimamia
manzuki.
• Kutunza
hifadhi za nyuki.
• Kukusanya
takwimu za ufugaji nyuki.
• Kutunza
kumbukumbu za kazi za utafiti.
• Kuondoa
nyuki wanaodhuru binadamu na mifugo.
• Kutoa
leseni za biashara ya mazao ya nyuki.
• Kutoa
ushauri wa kitaalam kwa wananchi juu ya ufugaji endelevu wa nyuki na matumizi
bora ya mazao ya nyuki.
• Kutunza
makundi ya nyuki wanaouma na wasiouma.
7.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) au
Stashahada (Diploma) ya Ufugaji
Nyuki kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
7.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za
mishahara ya Serikali yaani TGS B na TGS kwa mwezi.
8.0 DOBI DARAJA LA II – NAFASI 1 (LINARUDIWA)
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya uchambuzi wa nguo kwa
ajili ya kuosha, kukausha, kunyoosha na kuzifungasha.
8.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au
mitatu katika fani ya Dobi (Laundry
Services) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
8.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya
Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS. C kwa mwezi.
9.0 MTUNZA BUSTANI DARAJA LA II - NAFASI 3 (LINARUDIWA)
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kupanda
maua katika maeneo yanayohusika.
• Kupanda
na kukata majani na kumwagilia maji.
• Kupanda
mboga, matunda katika bustani.
• Kupalilia
mazao katika bustani.
• Kufanya
kazi zingine zitakazoelekezwa na Viongozi wa Kitengo chao.
9.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti katika
fani ya utunzaji bustani za maua, mboga na upandaji majani kutoka chuo cha
Maendeleo ya Wananchi, VETA, au JKT au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya
Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
10.0 AFISA WA SHERIA DARAJA LA II (LEGAL OFFICER
GRADE II) – NAFASI 3(LINARUDIWA)
10.1 MAJUKUMU YA KAZI
Hili ni daraja la mafunzo katika
kazi, hivyo Maafisa wa Sheria katika daraja hili watafanya kazi za kisheria kwa
maelekezo ya Maafisa wa Sheria Waandamizi ikiwa ni pamoja na:
• Kutoa
ushauri na kufanya utafiti wa kisheria pale anapohitajika kulingana na Wizara,
Idara ya Serikali ama sehemu aliko.
• Kufanya
mawasiliano na ofisi nyingine kuhusu masuala ya kisheria kwa maelekezo ya
Maafisa wa Sheria walio katika ngazi za juu.
10.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya
kwanza ya Sheria kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na waliomaliza
mafunzo ya uwakili yanayotambuliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
10.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E Kwa mwezi
11.0 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) -
NAFASI
10(LINARUDIWA)
11.1 MAJUKUMU YA KAZI
•
Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za
uhasibu.
Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu
Kupeleka
barua/nyaraka za uhasibu Benki.
•
Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za
Benki na Amana.
11.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC
level II au “Foundation Level” kinachotolewa na NBAA
11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya
Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi
12.0 MWENYEKITI WA MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA
YA WILAYA
(CHAIRPERSON)
– NAFASI 1.-INARUDIWA
Nafasi hizi ni kwa ajili ya
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi.
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kusikiliza,
kuamua migogoro yote ya Ardhi na Nyumba kwa mujibu wa Sheria
Na 2 ya mwaka 2002 inayohu Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya
Wilaya Kusikiliza
na kutoa uamuzi wa Rufaa kutoka Mabaraza ya Kata
Kufanya marejeo kwa mashauri yaliyosikilizwa na mabaraza ya Kata.
• Kusimamia
utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya na
•
Mabaraza ya Kata katika eneo husika.
12.2
SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa
wenye Shahada ya Sheria na kuendelea kutoka Chuo kikuukinachotambulika na
serikali na kumaliza mafunzo ya kazini (internship)
• Awe
na uzoefu wa miaka mitano (5) katika masuala ya Sheria na Kutoleauamuzi
• Awe
mwadilifu na asiye na historia ya makosa ya jinai
•
Awe na umri usiopungua miaka 35
12.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya
Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.J kwa mwezi.
13.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (MAJI) (ASISTANT
TECHNICIAN - WATER) NAFASI 2(LINARUDIWA)
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kupima
uwingi wa maji mtoni
• Kusoma
kituo cha hali ya hewa
• Kazi
nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
13.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato
cha VI waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka kutoka Chuo cha
Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi
Daraja la III katika fani ya maji.
13.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
14.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - UMEME (TECHNICIAN
GRADE II ELECTRICAL) – NAFASI 4(LINARUDIWA)
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya
ukaguzi wa ubora wa magari ya Serikali na kurekebisha ipasavyo.
• Kufanya
upimaji wa Mitambo na Umeme kufuatana na Maelekezo ya Mhandisi.
• Kufanya
kazi za kutengeneza magari,na vifaa vya
Umeme
• Kufanya
usanifu wa miradi midogo midogo ya umeme
• Kusimamia
jinsi ya kufunga mashine mpya zinazowekwa kwenye karakana za ufundi na Umeme.
14.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa
zilizotajwa hapa chini:
• Waliohitimu
kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya ufundi Umeme.
• Waliohitimu
kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi
vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya ufundi Umeme,
• Wenye
Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi
kinachotambuliwa na Serikali,
• Wenye
Stashahada ya Kawaida katika fani ya ufundi Umeme kutoka Chuo kinachotambuliwa
na Serikali.
14.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
15.0 MCHAPA HATI DARAJA LA II – NAFASI
1(LINARUDIWA)
15.1 MAJUKUMU YA KAZI
•
Kuchapa taarifa za Uthamini na Hati za fidia
•
Kuchapa Nyaraka na Hati za kumiliki ardhi
15.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au cha Sita waliofaulu
mtihani wa Uhazili Hatua ya II kutoka Chuo cha Watumishi wa Umma na ujuzi wa
Kompyuta Hatua ya I na II kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
15.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B
16.0 KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL
SECRETARY GRADE III) – NAFASI 30(LINARUDIWA)
16.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kuchapa
barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
• Kusaidia
kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza
kushughulikiwa.
• Kusaidia
kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari
za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa wakati unaohitajika.
• Kusaidia
kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote
kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
• Kusaidia
kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu
kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia
kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na
kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
• Kutekeleza
kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
16.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato
cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya
Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato
ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo
ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti
katika programu za Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
16.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
17.0 FUNDI SANIFU MAABARA MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY
LABORATORY TECHNICIAN II) – NAFASI 5(LINARUDIWA)
17.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kwa
kushirikiana na Afisa Mifugo Msaidizi, atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo
katika eneo lake.
• Atakusanya
sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa maabara.
• Kuwasaidia
wataalam kuanda vifaa vya uchunguzi
• Kutunza
Usafi wa Maabara na vyombo vilivyomo.
• Kutunza
takwimu za uchunguzi
•
Atafanya kazi zingine zozote kama atavyopangiwa na
mkubwa wake wa kazi
17.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha sita (VI) waliofuzu mafunzo ya miaka miwili
(2) ya Stashahada katika fani ya Fundi Sanifu Maabara (Mifugo) kutoka Chuo cha
Mifugo (LITI), au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
17.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi
18.0 MSAIDIZI USTAWI WA JAMII II (SOCIAL WELFARE
ASSISTANT) – NAFASI 2 (LINARUDIWA)
18.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kutambua
na kuhudumia watu walio katika makundi maalum na mazingira hatarishi
• Kukusanya
takwimu zinazohusu watu walio katika makundi maalum na mazingira hatarishi
• Kuchambua
na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye
dhiki
•
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa
kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake
18.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita na wenye cheti cha mafunzo ya
mwaka mmoja ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
18.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C Kwa mwezi.
19.0 MTHAMINI DARAJA LA II (VALUER GRADE II) – NAFASI 7(LINARUDIWA)
19.1 MAJUKUMU YA KAZI
•
Kukusanya taarifa za utafiti na mwenendo wa soko la
ardhi.
•
Kuhakiki kumbukumbu za utafiti na kuziingiza kwenye
kompyuta
19.2
SIFA ZA MWOMBAJI
•
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika fani
ya Usimamizi Ardhi na
Uthamini (Land management and Valuation)
kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi au Taasisi nyingine zinazotambuliwa na Serikali
katika fani za Usimamizi Ardhi na Uthamini. Au
•
Kuajiriwa wenye cheti cha NCPS katika fani ya Usimamizi
Ardhi na Uthamini.
19.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi.
20.0 FUNDI SANIFU DARAJA II - UPIMAJI NAFASI 3(LINARUDIWA)
20.1 MAJUKUMU YA KAZI
Sehemu
ya Topographic and Geodetic Survey:
Kupanga na kuandaa mahitaji ya
kambi za upimaji, vifaa vya upimaji na mahitaji ya jumla.
20.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Diploma ya
kawaida katika fani ya Upimaji Ardhi, kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
na wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitano.
20.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
21.0 MKUFUNZI MSAIDIZI DARAJA LA II–HOME
ECONOMICS/ DOMESTIC SCIENCE
(NAFASI
4)(LINARUDIWA)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Wakufunzi wasaidizi hawa
watafanya kazi ya kufundisha somo la ushonaji, ufumaji, kudarizi, upishi na
lishe katika vyuo vya maendeleo ya wananchi Tanzania Bara
21.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufundisha
masomo ya ushonaji, ufumaji, kudarizi na upishi na lishe katika vyuo vya
maendeleo ya wananchi.
• Kutayarisha
mpango wa kazi wa Mafunzo
• Kupima
Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
• Kutunza
vifaa vya kufundishia
• Kufanya
na kutoa taarifa za Utafiti
• Kutoa Ushauri wa kitaalam
• Kuandaaa
kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
• Kutunga
na kusahihisha Mitihani
• Kufanya
Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/hangamoto mbalimbali katika jamii
inayoizunguka chuo
•
Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na
kuendeleza Mafunzo nje ya chuo
21.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu mafunzo ya stashahada ya
ufundi katika fani zaushonaji, ufumaji, kudarizi, upishi na lishekutoka vyuo
vya ufundi vinanvyotambuliwa na Serikali.
21.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS Ckwa mwezi.
22.0 MKUFUNZI MSAIDIZI DARAJA LA II- ELECTRICAL
ENGINEER - (NAFASI 10) (LINARUDIWA)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Wakufunzi hawa watafanya
kazi ya kufundisha somo la Umeme wa majumbani (Electrical installation),
computer application na technical drawing katika vyuo vya maendeleo ya Jamii
Tanzania Bara
22.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufundisha
somo la umeme wa majumbani, computer application na technical drawing katika
vyuo vya maendeleo ya wananchi.
• Kutayarisha
mpango wa kazi wa Mafunzo
• Kupima
Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
• Kutunza
vifaa vya kufundishia
• Kufanya
na kutoa taarifa za Utafiti
• Kutoa Ushauri wa kitaalam
• Kuandaaa
kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
• Kutunga
na kusahihisha Mitihani
• Kufanya
Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/hangamoto mbaimbali katika jamii
inayoizunguka chuo
• Kutoa
Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya chuo
22.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato
cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya stashahada katika fani ya Umeme kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
22.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
23.0 MKUFUNZI DARAJA LA II- MHANDISI UJENZI
(CIVIL ENGINEER)-(NAFASI 4)(LINARUDIWA)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Wahandisi hawa watafanya
kazi ya kufundisha somo la Ujenzi katika vyuo (24) vya maendeleo ya Wananchi na
chuo cha Maendeleo ya Jamii Missungwi
23.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufundisha
somo la uungaji vyuo, computer application na Technical drawing katika vyuo
vyuo vya maendeleo ya wananchi.
• Kutayarisha
mpango wa kazi wa Mafunzo
• Kupima
Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
• Kutunza
vifaa vya kufundishia
• Kufanya
na kutoa taarifa za Utafiti
• Kutoa Ushauri wa kitaalam
• Kuandaaa
kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
• Kutunga
na kusahihisha Mitihani
• Kufanya
Utafiti utakaosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbaimbali katika
jamii inayoizunguka chuo
• Kutoa
ushauri juu ya kuboresha taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya chuo
23.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato
cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/ stashahada ya juu katika fani ya
Uhandisi Majengo(Civil Engeneering) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na
Serikali
23.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS Dkwa mwezi.
24.0 MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 1
(LINARUDIWA)
24.1 MAJUKUMU YA KAZI
•
Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.
•
Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi
wa wageni wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.
Kupokea na kusambaza maombi ya
simu za ndani.
•
Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi
zake.
•
Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi
watakakopewa huduma.
•
Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi
(Appointment) au wamepata idhini ya maafisa husika.
•
Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa
mbalimbali ofisini.
•
Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje
ya ofisi.
•
Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya
ofisi na zinazopigwa kwenda nje.
24.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato
cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati na kufuzu mafunzo
ya Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
24.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
25.0 MHANDISI II
UFUNDI (MECHANICAL ENGINEER) – NAFASI 20
25.1 MAJUKUMU YA KAZI
•
Kufanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi
aliyesajiliwa na bodi ya usajili wa Wahandisi kama Professional Engineer ili
kupata uzofu unaotakiwa.
•
Kufanya kazi kwa vitendo katika fani ya Mekanika ili
kumwezesha kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.
•
Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu magari na mitambo
mbalimbali, bei za magari na mitambo na vifaa vya umeme ndani na nje ya nchi.
•
Kupitia mapendekezo ya miradi (project proposals)
mbalimbali ya Ufundi .
25.2
SIFA ZA MWOMBAJI
•
Kuajiriwawenye Shahada/Stashahada ya juu ya Uhandisi
(Mechanical Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambulika na Serikali.
25.3
MSHAHARA
•
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS Ekwa mwezi.
26.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MITAMBO (TECHNICIAN GRADE II
MECHANICAL)
– NAFASI 4(LINARUDIWA)
26.1
MAJUKUMU YA KAZI
•
Kufanya ukaguzi wa ubora wa magari ya Serikali na
kurekebisha ipasavyo.
•
Kufanya upimaji wa Mitambo kufuatana na Maelekezo ya
Mhandisi.
Kufanya kazi za kutengeneza mitambo na magari
•
Kufanya usanifu wa miradi midogo midogo ya mitambo
•
Kusimamia jinsi ya kufunga mashine mpya zinazowekwa
kwenye karakana za ufundi .
26.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa
zilizotajwa hapa chini:
•
Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi
ya miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya ufundi
Mitambo.
•
Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya
miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika
fani ya ufundi Mitambo,
•
Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka
Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
•
Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani ya ufundi
Mitambo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
26.3
MSHAHARA
•
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS
C kwa mwezi
27.0 AFISA ELIMU DARAJA LA II –NAFASI 1
27.1 MAJUKUMU YA KAZI
•
Kufundisha katika Chuo cha Madini Dodoma kufuatana na
masomo aliyosomea.
•
Kuandaa maazimio ya kazi, maandalio ya masomo, zana za
kufundishia/kujifunzia,mazoezi ya wanafunzi na wanachuo.
•
Kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani kwa lengo la
kutathmini maendeleo ya wanafunzi na wanachuo.
•
Kuandaa,kuwapangia kazi wanafunzi/wanachuo na
kusahihisha mazoezi
•
Kuandaa taarifa kuhusu kazi za wanafunzi/wanachuo
nakuwasilishwa kwa uongozi wa shule/chuo.
•
Kuandaa na kutunza kumbukumbu za wanafunzi/wanachuo na
kuwasilishwa katika mamlaka husika.
•
Kufanya tafiti mbalimbali za kielimu
•
Kusimamia vyama vya masomo(Association).
•
Kushika zamu na kutoa taarifa kwa uongozi wa shule/chuo
•
Kusimamia”clubs” za masomo
•
Kuandaa mpango kazi na kutoa kipaumbele kwa majukumu
kulingana na upatikanaji wa nyenzo.
•
Kutunza na kudhibiti matumizi ya vifaa katika sehemu
aliyokabidhiwa
Kufanya shughuli za ukuzaji mitaala
Kazi nyingine atakazopangiwa na
Mkuu wa Kituo
27.2
SIFA ZA MWOMBAJI
•
Kuajiriwa wenye Shahada ya Elimu katika fani ya Hesabu
na Sayansi ya Kompyuta(Computer Science) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam au vyuo vingine vingine
vinavyotambuliwa na Serikali
27.3
MSHAHARA
•
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGTS.D kwa mwezi
X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma.