Dereva wa Mitambo Daraja la II (Plant Operators)-X 4

Dereva wa Mitambo Daraja la ii (Plant Operators) (nafasi 04)

sifa za mwombaji:
Kuajiriwa kwa mkataba wenye cheti cha kidato cha iv ambao wana leseni daraja la "g" ya kuendesha mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo hiyo, wenye uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda usiopungua saa mia tatu (300) au miezi mitatu (3) bila kusababisha ajali.

majukumu ya kazi
Kuendesha mitambo chini ya usimamizi wa dereva mitambo mwenye uzoefu.

Mshahara
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya serikali kwa mujibu wa muundo wa utumishi wa kada ya madereva wa mitambo (plant operators) - tgos a.
Masharti ya jumla kwa madereva na maopereta wa mitambo
I)waombaji wote wawe ni raia wa tanzania wenye umri kuanzia miaka 18
Na wasiozidi umri wa miaka 45.
Ii) waombaji w.ote waambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa .
Iii) waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza
(detailed cv) yenye anwani na namba za simu za kuaminika, nakala ya
Leseni husika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
Kuaminika
Iv) picha mbili "passport size" za hivi karibuni na ziandikwe jina kwa nyuma.
V) "testimonials","provisional results", "statement of results", hati ya matokeo ya kidato cha nne "result slip" havitakubaliwa.
vi) waombaji waliostaafishwa katika utumishi wa umma hawaruhusiwi
Kuomba isipokuwa tu kama wana kibali cha katibu mkuu kiongozi
Vii) maombi vote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, kidato cha nne pamoja na vyeti vya mafunzo mbalimbali vinavyohusika. Viambatanisho vyote vibanwe na barua kwa pamoja kuondoa uwezekano wa kupotea.
Viii) mwisho wa kupokea barua za maombi ni siku ya jumatatu, tarehe 11 aprili, 2016 saa 9:30 mchana.
Ix) uwasilishaji wataarifazakugushi utaadhibiwakisheria;a'idha, maombi
Vote yaandikwe kwa lugha ya kiswahili au kiingereza na yanaweza
Kuwasilishwa moja kwa moja masjala ya manispaa, ya dodoma au
Kutumwa kupitia posta kwaanuaniifuatayo:


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Mkurugenzi wa manispaa,
Halmashauri ya manispaa,
S.L.P 1249
Dodoma