NAFASI ZA KAZI KATIKA KITUO CHA JAMII CHA CKC KING’ORI

Kituo cha jamii cha ckc King’ori kinaalika barua za maombi ya kazi kutoka kwa waombaji ambao wana uwezo na uzoefu wa kutosha katika fani ya kompyuta ili waweze kuungana nasi katika kuelimisha jamii kwa njia ya elimu ya teknolojia na mawasiliano.


MKUFUNZI DARAJA LA II- COMPUTER SCIENCE (NAFASI 2) 

Wahandisi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la computer na electronics (Computer Application) katika chuo cha CKC KING’ORI kilichopo wilaya ya MERU MKOANI ARUSHA.

MAJUKUMU NA KAZI

§  Kufundisha somo la computer na electronics.

§  Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo

§  Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo

§  Kutunza vifaa vya kufundishia

§   Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti

§   Kutoa Ushauri wa kitaalam

§   Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni

§  Kutunga na kusahihisha Mitihani

§  Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/Changamoto mbalimbali katika jamii inayoizunguka chuo

§  Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya chuo 

§  Kufanya shughuli mbali mbali za masoko na shughuli zingine zozote atakazopangiwa na mkuu wake wa kituo

SIFA ZA MWOMBAJI 

§  Mwombaji awe amehitimu kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/ stashahada katika fani ya computer science kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali

§  Awe na uzoefu wa kufundisha kompyuta kwa mda usiopungua miaka miwili

§  Mwombaji asiwe na zaidi ya umri wa miaka 30

§  Awe raia wa Tanzania

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI

Mwombaji aambatanishe nakala ya vyeti vyake ,CV(curriculum Vitae),pamoja na picha mbili za pasipoti size.

Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa anuani ifuatayo

CKC MANAGER,                     

P.O.BOX 670, USA-RIVER.                                                                      AU   kwa barua pepe ifuatavyo

                                                                                                                        kingorickc1@gmail.com                                 mwisho wa kupokea maombi ni  tarehe 25/7/2015