Madereva wa Magari(50) -Astashahada(NTA level 3 or 4 POSITION DESCRIPTION:

Jeshi la Polisi Tanzania linatangaza nafasi za ajira kwa mwaka wa fedha 2015/2016 kwa vijana wenye elimu ya vyuo vya elimu ya juu, waliosomea ujuzi/fani mbalimbali toka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wahitimu wa kidato cha sita wa mwaka 2014 waliopitia Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria.


ASTASHAHADA(NTA level 3 or 4

Mafundi Rangi za Magari (Spray Painting)

MASHARTI KWA MWOMBAJI
1. Mwombaji atajaza fomu ya maombi kikamilifu na atabandika
picha yake “Ppt Size” kwenye fomu.
2. Mwombaji aambatanishe katika fomu vivuli vya vyeti vyote
yaani cheti cha kuzaliwa, kuhitimu elimu ya sekondari[Leaving
& Academic], cheti/vyeti vya taaluma[Academic Transcript] na cheti cha
kumaliza Jeshi la kujenga taifa kwa wahitimu wa kidato cha sita.
3. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

SIFA ZA MWOMBAJI
1. Awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
2. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25 kwa wahitimu wa

astashahada, stashahada na kidato cha sita.
3. Kwa wahitimu wa shahada awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi

miaka 28.
4. Awe amehitimu chuo mwaka wa masomo 2014 tu.
5. Kwa wahitimu wa kidato cha sita awe amehitimu mwaka 2014 na kupitia

Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria
6. Awe na tabia njema.
7. Asiwe na kumbukumbu za kutenda uhalifu.
8. Awe na afya njema[kimwili na kiakili]
9. Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.

10. Asiwe na alama za kuchora mwilini[tatuu].
11. Awe na urefu usiopungua sentimita 155 futi tano nchi mbili
12. Asiwe mtumiaji wa madawa ya kulevya.
13. Awe hajaajiriwa na idara nyingine Serikalini.
14. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Polisi.
15. Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje ya Tanzania


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Wahusika watajaza fomu baada ya kujazwa kikamilifu wataambatanisha vivuli vya vyeti na kutuma Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa njia ya Posta kabla ya tarehe 30/06/2015. Kwa anuani ifuatayo:
Inspekta Jenerali wa Polisi,

Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM

Imetolewa na
Makao Makuu ya Polisi(T)
DAR- ES- SALAAM.