Ref. Na EA.7/96/01/H/ 63 31-Julai, 2015

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 435 za kazi kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili.

MHAKIKIMALI  DARAJA II- NAFASI 22

Nafasi hizi ni kwa ajili ya  Katibu Mkuu wizara ya Fedha

19.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kukagua bohari za kati za Serikali na kutoa taarifa za ukaguzi

Kutathimini na kuchambua hoja muhimu zilizomo katika taarifa za uhakiki

Kufanya uchambuzi wa taarifa za “Boards of Survey” na kutoa mapendekezo juu ya utekelezaji wake

Kutunza daftari la taarifa za upotevu, ajali, fidia, vitunzia fedha (cash receptacles), usajili wa magari ya Serikali na uhalalisho (retrospective approval)

19.2 SIFA ZA MWOMBAJI

kuajiriwa wenye Stashahada ya Juu katika fani ya ugavi (materials managent) au shahada/stashahada ya juu ya biashara katika ununuzi wa vifaa/ugavi, kutoka chuo/taasisi inayotambuliwa na serikari au

wenye “professional level ii/iii” inayotolewa na bodi ya taifa ya usimamizi wa vifaa (NBMM), au sifa inaylingana na hiyo inayotambuliwa na bodi

na wawe na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu (3).

waombaji wenye “certified supplies professiona” (CSP) inayotolewa na bodi ya taifa ya usimamizi wa vifaa (NBMM) au sifa inayolingana na hiyo inayotambuliwa na bodi hiyo watafikiriwa kwanza.

19.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGS. D kwa mwezi.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/

(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv. Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed

C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.


- Postgraduate/Degree/Advanced

Diploma/Diploma/Certificates.

- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

- Computer Certificate

- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Agosti, 2015

xii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza .

MUHIMU; Waombaji kazi wote mnatahadharishwa kujiepusha na matapeli wanaojitambulisha kama watumishi wa Sekretarieti ya ajira kuomba Rushwa kwa baadhi ya waombaji kazi ili kuwapangia vituo vya kazi.