Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu
waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe
29/07/2015 hadi tarehe 30/07/2015 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo
vya kazi umekamilishwa.

Nafasi za kazi NECTA Nafasi ziko Nyingi


Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi ni kama yanavyoonekana
katika Tangazo hili. Katika orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi
ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Data base) kwa kada
mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi
kupatikana.

Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika
muda ambao umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi
wakiwa na vyeti halisi (Original Certificates) vya masomo kuanzia kidato
cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya
ajira. Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao za
posta.

Nafasi za Kazi SWISSAID Tanzania


Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa
mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

KUITWA KAZINI AUGUST 2015 (Placements)