Ref. Na EA.7/96/01/H/ 63 31-Julai, 2015


Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 435 za kazi kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili.

15.0 KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III 50

15.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.

Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.

Kusaidia kutunza taarifa / kumbukumbu zamatukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba na kazi zingine. Zilizo pangwa kutekelezwa katika ofisi anamo fanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwawakati unao hitajika.

Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinacho hitajika katikashughulizakazihapoofisini.

Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.

Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya , kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazo husika.

Kutekeleza kazi zozote atakazo kuwa amepangiwa na Msimamizi wake wakazi.

15.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu.

Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika program za Windows, Microsoft Office,

Internet, E-mail naPublisher.

15.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/

(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv. Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed

C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

- Postgraduate/Degree/Advanced

Diploma/Diploma/Certificates.

- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

- Computer Certificate

- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Agosti, 2015

xii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza .

MUHIMU; Waombaji kazi wote mnatahadharishwa kujiepusha na matapeli wanaojitambulisha kama watumishi wa Sekretarieti ya ajira kuomba Rushwa kwa baadhi ya waombaji kazi ili kuwapangia vituo vya kazi.