Ref. Na EA.7/96/01/H/ 63 31-Julai, 2015


Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 435 za kazi kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili.

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara, Halmashauri pamoja na Taasisi mbalimbali serikalini.

12.0 AFISA MIFUGO MSAIDIZI DARAJA LA II (LIVESTOCK FIELD OFFICER II) –

NAFASI 20

12.1 MAJUKUMU YA KAZI

Atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji wa eneo lake.

Kwa kushirikiana na wakaguzi wa afya, atakagua nyama na usafi wa machinjio

mara kwa mara.

Atakusanya takwimu za nyama na mazao yatokanayo na mifugo k.m ngozi na

kuandika ripoti.

Atatibui magonjwa ya mifigo chini ya usimamizi wa Daktari wa mifugo na

kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa.

Atatembelea wafugaji mara Kwa mara na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalam
katika eneo Lake Kazi.

Atakusanya takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo lake.

Atashauri na kusimamia ujenzi wa majosho, machinjio, vibanio na miundo mbinu

inayohusiana na ufugaji bora.

Atahusika na uhamilishaji (Artificail Insemination) na uzalishaji (breeding) wa

mifugo kwa ujumla.

Atashauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha maziwa na utunzaji wa

ndama.

Atafanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa

kazi.

12.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha VI waliofuzu mafunzo ya Stashahada

(Diploma) ya mifugo kutoka chuo cha Kilimo na Mifugo (MATI au LITI) au chuo

kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.

12.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/

(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv. Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed

C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.


- Postgraduate/Degree/Advanced

Diploma/Diploma/Certificates.

- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

- Computer Certificate

- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Agosti, 2015

xii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza .

MUHIMU; Waombaji kazi wote mnatahadharishwa kujiepusha na matapeli wanaojitambulisha kama watumishi wa Sekretarieti ya ajira kuomba Rushwa kwa baadhi ya waombaji kazi ili kuwapangia vituo vya kazi.