JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Ref. Na EA.7/96/01/H/ 63 31-Julai, 2015
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 435 za kazi kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili. Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara, Halmashauri pamoja na Taasisi mbalimbali serikalini.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Agosti, 2015
xii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza . MUHIMU; Waombaji kazi wote mnatahadharishwa kujiepusha na matapeli wanaojitambulisha kama watumishi wa Sekretarieti ya ajira kuomba Rushwa kwa baadhi ya waombaji kazi ili kuwapangia vituo vya kazi.

7.0 MKADIRIAJI UJENZI (QUANTITY SURVEYORS)-NAFASI-6
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kuandaa ratiba ya kazi, gharama za ujenzi (BOQ) na Hati za mikataba.
• Kuanda makisio ya gharama za miradi ya Ujenzi.
• Kukusanya takwimu na kufanya uchunguzi ( survey)ya ukarabati wa miradi ya Ujenzi
• Kuandaa bajeti ya miradi ya ujenzi
• Kuandaa taarifa za uthamini wa miradi ya ujenzi.
• Kwa kushirikiana na Mkadiriaji ujenzi kuandaa taarifa fupi za ujenzi wa miradi.
• Kushughulikia masuala yote ya utawala wa fedha za miradi kuandaa hati / vibali maalumu vya ujenzi na mikataba.
• Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Shahada /Stashahada ya juu ya Uhandisi kutoka vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya Ukadiriaji Ujenzi (quantity Surveryor).
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.



TUMA MAOMBI KUPITIA--------->

============
Job Category
Other
Industry
Government
Qualifications
Awe na Shahada /Stashahada ya juu ya Uhandisi kutoka vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya Ukadiriaji Ujenzi (quantity Surveryor).
Experience
NONE
Company Name
TAASISI YA SERIKALI
Apply To
http://portal.ajira.go.tz/
CITY
Dar es salaam
Country
Tanzania
Email
http://portal.ajira.go.tz/
Deadline
14TH AUGUST, 2015