HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe anatangaza nafasi ishirini na tatu(23) za kazi . maombi ya kujaza nafasi yoyote kati ya hizo yanakaribishwa kutoka kwa mtanzania yeyote mwenye sifa hizo zilizotajwa katika tangazo hili
Nafasi zilizotangazwa ni kama ifuatavyo
3.    KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III : (NAFASI 3) 
Majukumu:
i.    Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za akwaida.
ii.    Kusaidia kupokea wageni na kuwasai1i shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughu1ikiwa.
iii.    Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni,
tarehe za vikao, safari na Mkuu wake na ratiba zingine za kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
iv.    Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi na kumuarifu kuhusus taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao
v.    Kutekeleza kazizozote atakazopangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

Mwombaji awe na sifa zifuatazo:-
i.    Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Sita(VI)
ii.    Awe amahitimu mafunzo ya Uhazili kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma au Chuo chochote kinachojarnbuliwa na Serikali.
iii.    Awe amefaulu somo la Hati Mkato na mwenye uwezo wa kuchapa maneno themanini kwa dakika moja na
iv.    Awe amesoma masomo ya computer,

Ngazi ya Mshahara: TGS B
Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
xvii.    Mwombaji awe raia wa Tanzania
xviii.    Awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18.
xix.    Maombi yote yaambatanishwe na nakala ya cheti cha Taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha nsie] sita, Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu (3) wa kuaminika na picha mbili (passport size) za hivi karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma)
xx.    Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha Nne/ Sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au wakili anayetambulika na Serikali. Aidha atakayewasilisha taarifa na sifa za kugushi atachukuliwa hatua za Kisheria na mamlaka zinazohusika.
xxi.    Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu, maombi yake hayatashughu1ikiwa.
xxii.    Watumishi ambao wa1ikwisha kuajiriwa hapo awali Serikalini na kupangiwa vituo vya kazi maeneo mengine wasiombe nafasi hizi za kazi kwa kuwa hawataweza kuingia kwenye Payroll ya Serikali.
xxiii.    Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
xxiv.    Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta, maombi yatakayowasilishwakwa mkono au barua pepe
hayatafanyiwa kazi:
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta kupitia anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
S.L.P. 01
MASUMBWE
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/07/2015, Saa 9:30 Alasir.
Abdallah l. Mfaume
Mkurugeozi Mtendaji (W)
MBOGWE
SOURCE; MWANANCHI 09TH JULY 2015
============
Job Category
Other
Industry
Government
Qualifications
Awe amahitimu mafunzo ya Uhazili kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma au Chuo chochote kinachojarnbuliwa na Serikali.
Experience
NONE
Company Name
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE
Apply To
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
P O BOX
01, MASUMBWE
CITY
Shinyanga
Country
Tanzania
Deadline
31/07/2015,