HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALATANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala-Kahama anapenda kuwatangazia wote wananchi wote wenye sifa kuomba nafasi mbalimbali za kazi mbalimbali kama ifuatavyo
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 4)
Muombaji awe na sifa zifiatazo
•    Awe amehitimu kidato cha Ne (IV) au Sita (VI)
•    Awe amehitimu mafunzo ya Cheti cha Utunzaji Kumbukumbu
•    Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
KAZI NA MAJUKUMU
•    Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na maafisa
•    Kuthibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka
•    Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi
•    Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinet) katika masjala
•    Kuweka kumbukumbu(barua/nyaraka nk) katika mafaili 
Ngazi ya mshahara; TGS B
VIGEZO NA MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI 
•    mwaombaji awe raia wa Tanzania
•    awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18
•    Maombi yote yaambatanishwa na nakala za cheti cha kuhitimu taaluma , nakala ya cheti cha kidato cha Nne/sita, maelezo binafsi yanayojitoshereza (CV) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu na picha mbili (Passport size) za hivi karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma) 
•    Vyeti vyote vya taaluma na kidato cha Nne/Sita ni lazima vithibitishwe na hakimu au wakili anayetambulika na serikali. Aidha uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria
•    Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa
•    Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili/Kiingereza
Barua zote zitumwe kwa njia ya posta, maombi yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayatafanyiwa kazi
 Maombi yote yatumwe kwa anwani ifuatayo
MKURUGENZI MTENDEJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA
S.L.P 16
KAHAMA
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI ALHAMISI TAREHE 30/07/2015 
SOURCE; NIPASHE 17TH  JULY 2015
KUTUMA MAOMBI -------------->
 
============

Job Category
Other
Industry
Government
Qualifications
Awe amehitimu mafunzo ya Cheti cha Utunzaji Kumbukumbu
Experience
NONE
Company Name
HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA
Apply To
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
P O BOX
16 , KAHAMA
CITY
Shinyanga
Country
Tanzania
Deadline
30th July 2015