HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALATANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala-Kahama anapenda kuwatangazia wote wananchi wote wenye sifa kuomba nafasi mbalimbali za kazi mbalimbali kama ifuatavyo
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III(NAFASI 39)
Muombaji awe na sifa zifiatazo
•    Awe amehitimu kidato cha Ne (IV) au Sita (VI)
•    Awe amehitimu mafunzo ya cheti/Astashahada katika moja ya fani zifuatazo; Utawala, sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali
KAZI NA MAJUKUMU
•    Utakua mhamasishaji wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji mali, kuondoa njaa na umaskini
•    Utakua mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji
•    Utaratibu na kusimamia upangaji wa mipango shirikishi ya maendeleo ya vijiji na vitongoji
•    Utatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika kijiji
•    Kusimamia utendaji kazi wa wataalam na watendaji wengine katika ngazi ya kijiji
•    Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa katibu tarafa
•    Utakua msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji na vitongoji
Ngazi ya mshahara; TGS B
VIGEZO NA MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI 
•    mwaombaji awe raia wa Tanzania
•    awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18
•    Maombi yote yaambatanishwa na nakala za cheti cha kuhitimu taaluma , nakala ya cheti cha kidato cha Nne/sita, maelezo binafsi yanayojitoshereza (CV) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu na picha mbili (Passport size) za hivi karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma) 
•    Vyeti vyote vya taaluma na kidato cha Nne/Sita ni lazima vithibitishwe na hakimu au wakili anayetambulika na serikali. Aidha uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria
•    Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa
•    Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili/Kiingereza
Barua zote zitumwe kwa njia ya posta, maombi yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayatafanyiwa kazi
 Maombi yote yatumwe kwa anwani ifuatayo
MKURUGENZI MTENDEJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA
S.L.P 16
KAHAMA
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI ALHAMISI TAREHE 30/07/2015 
SOURCE; NIPASHE 17TH  JULY 2015

KUTUMA MAOMBI ----------> 

============