DAR ES SALAAM REGIONAL VOCATIONAL TRAINING AND SERVICES CENTRE
(DSMRVTCS)
TANGAZO LA KAZI
NAFASI ZA KAZI KWA MADEREVA (300)
Mradi wa mabasi yaendayo haraka (Articulated 18M na Ridid 12m) unatarajia kuanza utekezaji kuanza utekelezaji wake mwezi wa tisa mwaka huu, 2015
Mradi huu unasimamiwa na kampuni ya UDA Rapid Transit Limited (UDA-RT) ambayo ni kampuni iliyoundwa na Shirika la Usafirishaji Dar es salaam (UDA) kwa kushirikiana na wamiliki wa Daladala Jijini Dar es salaam (DARCOBOA na UWADAR). Mradi huu unahitaji kuajiri madereva wasiopungua 300 wenye uzoefu wa kuendesha magari ya abiria. Madereva wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo;

Sifa za muombaji
i.    Awe na umri kuanzia miaka thelathini (30) hadi miaka hamsini na tano
ii.    Awe na leseni halali ya daraja C, mwenye uzoefu usiopungua miaka miwili ya kuendesha magari ya abiria. Uzoefu wa kuendesha mabasi yenye urefu usiopungua mita 11 ni sifa ya ziada
iii.    Awe na leseni halali ya daraja la E yenye miaka isiyopungua miwili na awe na awe na uzoefu wa kuendesha magari makubwa yanayovuta tele
iv.    Ajue kuandika taarifa na kuweka kumbukumbuza kazi yake kwa ufasaha;
v.    Awe na afya njema, akili timamu, ari ya kufanya kazi kwa tija, mwadilifu, mbunifu na anayeweza kujisimamia mwenyewe katika kutimiza majukumu atakayopewa
vi.    Awe na wadhamini wanaoaminika na awe tayari kuchukuliwa alama za vidole
Waombaji watakaokua na sifa watashiriki majaribio ya awali ili kubaini uwezo wao kwa vitendo na nadharia na wale watakaokidhi viwango na vigezo vilivyowekwa watalazimika kuhudhuria mafunzo maalum ya wiki mbili, kuwanjengea umahiri wa kuyatumia magari hayo yaendayo kwa mwendo haraka
Udahili na mafunzo hayo yatatolewa na VETA, Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma Chang’ombe- Dar Es Salaam, kwa kushirikiana na Wataalamu wenye uzoefu wa miradi ya BRT kutoka China
Barua zote za maombi zitumwe kwa 
1.    Mkuu wa Chuo
DSM RVTSC
VETA
Chang’obe Road
SLP 40274
DAR ES SALAAM, TANZANIA
AU
2.    Zifikishwe ofisi za chuo cha VETA Chang’ombe, Barabara ya Chang’ombe au
3.    Barua pepe; This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 
MUHIMU; Udahili utaanza tarehe 06/07/2015 kwa maombi yatakayo tufikia mapeme na mafunzo ya kwanza yataanza tarehe 07/07/2015 na awamu ya tano nay a mwisho yatatolewa tarehe 31/08/2015. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/07/2015
SOURCE; MAJIRA 3RD JULY 2015